Sunday, February 3, 2013

RAISI JAKAYA MRISHO AWASILI MKOANI KIGOMA.

Raisi Jakaya akiwasili Mkoani Kigoma.
Akiwa wapungia mkono wananchi wa Kigoma.
Akiwasalimia wanachama wa NEC Mkoa wa Kigoma.
Hawa ni baadhi ya wananchi waliokuja kumlaki uwanja wa ndege.


MAMBO YA KANGA MOKO HAYA













MASHABIKI WA LIGI KUU ENGLAND HII NI RATIBA YA LEO.

West Brom vs Tottenham saa 16:30 ndani ya The hawthorns


Man city vs Liverpool saa 19:00 ndani ya Etihad stadium

VIONGOZI NA WANACHAMA WA CHADEMA WAJIUNGA NA NCCR MAGEUZI

Viongozi waandamizi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,pamoja na wanachama 15 wa cha hicho,wanatarajia kujiunga na chama cha NCCR Mageuzi kesho kwenye Hotel ya Double J jijini Mbeya.Viongozi wa CHADEMA wanatarajia kukutana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya NCCR Mageuzi na mshauri wa mambo ya kisiasa Danda Juju ambae atamwakilisha mwenyekiti wa chama hicho Bwana James MbatiaJuju ambae ameshawasili jijini Mbeya kwa ajili ya kuwaapisha viongozi hao wa CHADEMA,kutokana na lengo kua ni kusambaratisha chama hicho.Viongozi hao ambao wanatarajiwa kujiunga na chama cha NCCR Mageuzi ni pamoja na aliekua katibu mkuu wa mkoa CHADEMA  Bwana Eddo Makata,aliekua mwenyekiti wa Baraza la vijana CHADEMA{BAVICHA} Bi.Juliana Shonza na aliewahi kugombea ubunge mbozi mashariki ndugu Mtera Mwampamba

HAYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO.














KAMA SHABIKI WA KIGOMA ALL STARS HII INAKUHUSU.

Haya tena kwa wapenzi wa Kigoma all stars,sasa wanaandaa wimbo wao mpya utakaokujia hivi karibuni yote ni muendelezo wa ngoma kali mara baada ya kutamba na LEKA DUTIGITE sasa waja na ngoma yao mpya iitwayo NYUMBANI.
Kama ilivokua kwenye ngoma yao ya kwanza sasa waja kama awali tena na mjumuiko ule ule wa Linex,Baba Levo,Diamond,Chege,Queen Darling,Recho,Mwasiti,Ally kiba,Makomando,Ommy Dimponz n.k.kwenye ngoma hii inayoandaliwa na producer alieitengeneza ile ya awali ya Leka dutigite na ndio anaitengeneza na hii pia huyu si mwingine ila ni TUDDY THOMAS ndani ya NGOMA RECORD.
All the best KIGOMA ALL STARS.

BREAKING NEWS PPF TOWER YAWAKA MOTO.

Hili ndo jengo la PPF TOWER lililoko maeneo ya posta kwenye barabara ya OHAYO likionekana katika picha huku likifuka moshi .Moto huo umeonekana hasa ukiwaka kwenye ghorofa ya juu kabisa.
Watu wa zima moto wameshafika na wanaendelea na zoezi hilo na chanzo cha moto huo hakijajulikana ni nini.Ki ukweli zoezi hili ni gumu hasa kwa zima moto kutokana na urefu wa jengo lenyewe.taarifa zinazoendelea juu ya moto huo utazipata hapahapa,endelea kua nasi.