Thursday, July 7, 2016

PASSPORT ITAKAYOTUMIKA KUSAFIRIA NCHI ZA AFRICA YAZINDULIWA AFRIKA MASHARIKI.

Viongozi wa umoja wa nchi za Afrikakwenye vikao vyake umepanga kutambulisha matumizi ya passport moja tu itakayotumika katika nchi zote zaAfrika ili kurahisisha safari za ndani yaAfrika. Passport hiyo ya kielekroniki imepangwa kuzinduliwa wiki ijayo Kigali Rwanda.
Hii imekuwa ni mpango wa muda mrefu kuwa na passport moja katika bara la Afrika ifikapo mwaka 2020 ambapo ambapo utarahisisha kusafiri kwa waafrika wote bilioni 1.1  katika nchi zote 55 zaa bara la Afrika.
Mwenyekiti wa Tume ya umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma amesema mpango huo una lengo la kujenga umoja wa Afrika na kurahisisha safari za ndani na kuwezesha uhuru wa usafirishaji wa  bidhaa na huduma ndani ya bara la Afrika

MAKUSANYO YA MAPATO KWA MWAKA 2015/2016

July 05 2016 Mamlaka ya Mapato Tanzania imetoa taarifa ya makusanyo ya mwezi June ambao ni mwezi  unaofunga mwaka wa fedha 2015/2016. Kwa mwezi June pekee TRA imekusanya trilioni 1.4 na kwa mwaka wa fedha 2015/2016 wamekusanya zaidi ya trilioni 13.3 na kufikia lengo la makusanyo kwa mwaka huo la trilioni 13.36.

Saturday, July 4, 2015

Hali ya mwimbaji Banza Stone sio nzuri, imebidi apelekwe Hospitali akatibiwe..

unnamed IIHali ya kiafya ya Staa na mkongwe wa muziki wa dance Tanzania, Ramadhan Masanja aka Banza Stone sio nzuri, anaumwa kwa muda mrefu na wapo ambapo waliofikia hatua hata ya kumzushia mitandaoni kwamba amefariki.
Team ya millardayo.com ilifika nyumbani anapoishi, Sinza Dar es Salaam na kumkuta pamoja na ndugu zake, alikuwa anaumwa lakini aliongea pia kinachomsumbua.
unnamed IIINimeambiwa kwamba kwa sasa hali yake sio nzuri, imebidi ndugu wampeleke Hospitali Mwananyamala ili akapate matibabu zaidi.. nina picha pia akiwa Hospitali, na wapo waliojitokeza kwenda kumjulia hali.
unnamed 


Chanzo Millard Ayo.

NEW SONG;WISE DAMIAN ft B RANGER SIKILIZA NA KUDOWNLOAD HAPA


Aliripoti Polisi baada ya kutishiwa maisha na mchumba wake-Shamsa












Muigizaji wa filamu Shamsa Ford amefunguka na kusema kwamba tangu aachane na Ex boyfriend wake Dickson Matoke aliwahi kuwatishia kuwauwa yeye na mwanae zaidi ya mara 10.
Akizungumza na millardayo.com alisema…’Ni kweli wakati nilipokuwa katika mahusiano naye alikuwa ni mtu ambaye anapenda sana kuniambia neno nitakuuwa mimi na mwanangu ndio maana nilikuwa naogopa sana kwasababu nilihisi kuwa anaweza kufanya lolote kunikomoa na nilienda hadi polisi kuchukua RB yake ili kama lolote litakalotokea basi yeye atakuwa amehusika, yaani yule alikuwa ananiambia kabia yuko serious mbaya kuwa ataniuwa mimi na mtoto wangu lisha kwangu alikuwa anawaambia hata marafiki zangu ni mashahidi na mbaya zaidi alikuwa anasema hayo maneno na mbaya zaidi alikuwa anawaambia hata ndugu zake.
 
Shamsa akiwa na ex-boyfriend wake 
 Hayo maneno alikuwa anayaongea wakati bado niko naye kwenye uhusiano lakini ndio hivyo malumbano malumbano na mimi nilikuwa nimeshachoka na hizo tabia zake lakini baada ya kuachana naye ni vitisho labda anataka kumuona mtoto anatumia vitisho mara sasa ninapomnyima mtoto basi anatumia vitisho basi mimi nikikumbuka lile neon lake la kusema ataniuwa basi moyoni sina amani….’alisema

Friday, July 3, 2015

KAMA HUJABAHATIKA KUIONA VIDEO YA RIHANNA,NIMEKUWEKEA HAPA


Hii nyimbo ya Rihanna unaielewa vipi pindi ukiiangalia,toa mawazo yako hapa kwa kuandika comment yako hapa chini. BITCH BETTER HAVE MY MONEY BY RIHANNA



NEW SONG TOKA KWA EMINEM;KINGS NEVER DIE by EMINEM ft GWEN STEFANI,SIKILIZA HAPA

Eminem alikuwa kimya kwa muda lakini sasa amerudi tena kuziandika headlines zake kwenye ubao wa burudani. Eminem ameachia ngoma mpya wiki hii, ndani kamshirikisha msanii mwengine maarufu wa muziki wa Pop RnB Gwen Stefani.
Wimbo unaitwa Kings Never Die, na unaweza kuisikiliza hapa chini kwa kubonyeza Play



Pipi na mume wake wanatumia simu moja!? Mkasa wa Ally Nipishe na wizi!? #Hekaheka (Audio)


PIPILOO
Leo kwenye Hekaheka ya @CloudsFM alikuwepo Ally Nipishe, moja ya jamaa ambao waliwahi kufanya poa kwenye Bongo Fleva alafu baadae akawa kimya hivi, viko vingi vilitokea katikati na sisi hatukujua kuhusu hilo, leo ametoa majibu yote.
Staa mwingine aliyekuwepo ni Pipi, jina lake liko kwenye list ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri pia kwenye Muziki TZ… Ally kasimulia vingi ikiwepo ishu ya mikasa mbalimbali iliyomkuta, kuna wakati alikamatwa akafungwa jela baada ya kuhusishwa na wizi wa pesa.
Ishu ilianzia pale alipouziwa gari, kumbe lilikuwa ni gari ambalo liliibiwa na ndani yake kulikuwa na pesa pia.. mpenzi wake alihusika pia kumuunganisha na waliomuuzia gari hilo.
Pipi naye amezungumzia mambo mengi, kumbe yeye na mpenzi wake wanatumia simu moja…  yeye na mume wake wana misingi mizuri ya uaminifu, hawana mambo mengi kwa hiyo hawana sababu ya kufichana.
Nimekusogezea sauti yao hapa chini, bonyeza play kuisikiliza.

Chanzo,Millard Ayo.


Kazi anayotaka kufanya mtoto wa kwanza wa Obama yajulikana.

Mtoto wa kwanza wa rais wa Marekani Maria Obama ’17’ ameanza harakati zake za kutaka kuwa mwigizaji na muongozaji a filamu.
Malia ameonekana huko Brooklyn na kundi la watayarishaji na waigizaji wa “Girls” hivi karibuni huku mashabiki wakifahamishwa kuwa hatacheza kwenye filamu hii ila ndio anajifunza mambo hayo.
Malia alionyesha kupenda kuwa mwigizaji na hata kuonekana kwenye tamthilia ya Halle Berry “Extant.”



 

Wednesday, July 1, 2015

MKE AZUILIWA KWENDA KUMZIKA MUME WAKE,KISA KIKO HAPA

Hekaheka ya leo inatokea Shinyanga ambapo wanafamilia pamoja na majirani walimzuia mke wa marehemu kwenda kumzika mume wake kwa madai kuwa alikua akimnyanyasa enzi za uhai wake.
Wakati mume wake anafariki mama huyo hakuwepo na alipopigiwa simu kuwa mume wake amefariki alirudi nyumbani na kuwakuta ndugu wa mume wake na majirani wakiomboleza lakini yeye akionekana kutojali na macho yakiwa makavu na hakuwa na dalili ya huzuni.
Majirani wanasema aliwahi kumkana mume wake tangu zamani pamoja na kumtesa huku akiishi na mume mwingine ambaye ni mume wa mtu ndani ya nyumba ya mume wake huyo.
Wanandugu wa mume wakishirikiana na majirani na Mwenyekiti wa mtaa walimshusha kwenye gari mama huyo na watoto wake wakati wakienda kuzika kijijini kwao Bukoba na kuwaacha wenyewe.Chanzo clous fm.

ufisadi NACADA-KENYA

Mamlaka ya Taifa ya kupiga Vita Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya Kenya (Nacada) nchini Kenya,kupitia kwa mjumbe wake Charles Njagua alimaarufu kwa jina la Jaguar ameyasema hayo maraada ya kuyaona hayo mambo.
Jaguar ambaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Nacada karibu mwezi mmoja sasa, amesema amekuwa akikabiliwa na upinzani mkubwa kwa kuhoji upotevu na matumizi yasiyo sahihi ya fedha katika chombo hicho.
Akiongea katika mkutano kwenye ofisi Jaguar ambaye pia ni msanii wa muziki Kenya amedai kuwa wajumbe wa bodi ya Nacada na Kamati ya Fedha ni sehemu ya wahusika wa ubadhirifu wa fedha wa chombo hicho cha kupiga vita pombe na dawa za kulevya.
Jaguar amewatuhumu baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo kwa kuchota kiasi cha shilingi milioni 500 za Kenya bila ya kufanyiwa majadiliano na kuridhiwa na wajumbe wote wa bodi hiyo ya Nacada.

Matumizi ya gongo Rombo yapungua kwa 92% - DC

Unywaji wa pombe haramu ya gongo na ambazo hazina viwango umepungua kwa asilimiaa 92 wilayani Rombo baada ya serikali kukamata zana mbalimbali zinazotumika kutengezea pombe hiyo
Baadhi ya wanawake wa wilaya ya Rombo wakiandamana kuelekea kwa mkuu wa wilaya kama ishara ya kuunga mkono juhudi za serikali kupambana na matumizi ya gongo
Unywaji wa pombe haramu ya gongo na ambazo hazina viwango umepungua kwa asilimiaa 92 wilayani Rombo baada ya serikali kukamata mitambo 178, mapipa 3,500 ya malighafi, lita 550 za gongo, lita 108,000 za sumu za viwanda vya wazalishaji wakubwa wa pombe hizo kwa miezi mitatu iuliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembrise Kipuyo ametoa taarifa hiyo kwa mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo aliyepokea matembezi ya amani ya kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na upikaji na unywaji wa pombe hizo ambao unaathiri nguvu kazi yaliyoandaliwa na wanawake wa wilaya ya rombo...
Hata hivyo bw kipuyo ambaye anaongoza mapambano hayo baada ya kuhamia wilaya hiyo amesema, matembezi hayo yamempa nguvu na kasi mpya ya kupambana na wapikaji wakubwa wa pombe hizo ambao 58 kati yao wamekamatwa na kesi zao zinazoendelea mahakamani na wengine wamefungwa.
Katika taarifa yao wanawake hao wamewalaani baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaohamasisha unywaji na upikaji wa pombe hizo kwa kuiomba serikali ihalalishe gongo na kumtaka mkuu huyo wa wilaya asikatishwe tamaa na viongozi wa aina hiyo ambao ni wapinzani wa maendeleo.
Akipokea matembezi hayo ya kilomita mbili mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Wilbard Ringia amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ili kurejesha heshima ya kujieletea maendeleo kwa kufanya kazi kwa bidii ambayo imetoweka kutokana na unywaji wa pombe hizo.

chanzo EATV.

Witnesz: Ochu hajatangaza ndoa.

Baada ya kumsikia Witnesz jana katika kipindi cha Planet Bongo akikanusha juu ya uvumi kuwa hawezi kupata mtoto tena, staa huyo pamoja na mpenzi wake Ochu Sheggy wamefunguka juu ya ndoa yao hiyo.
msanii wa muziki wa bongofleva Witnesz akiwa na mchumba wake Ochu Sheggy
Witnesz amesema kuwa, kwa muda waliokaa pamoja mpaka sasa, kisheria wao ni kama mume na mke.
Diva huyo mkali wa michano ameeleza pia, kuhusiana na tukio la kufunga ndoa lenyewe linalotambulika kijamii, bado anamsubiri mumewe Ochu kuchukua hatua hiyo kutokana na kuwa yeye ndio muoaji.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE JUU YA MASHINE ZA BVR,IKO HAPA

Kama hukuwa karibu na redio yako,haya ndio aliyoyasema mh. Jakaya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania juu ya mashine za BVR sikiliza hapa na unaweza kuipakua pia.kwa hisani ya millard ayo.

Friday, June 26, 2015

MUSWADA WA HABARI WAONDOLEWA BUNGENI

Serikali imeuondoa muswaada wa sheria ya haki ya kupata habari uliokuwa uwasilisilishwe na kujadiliwa katika mkutano unaondelea wa bunge mjini Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na wizara maalum ambaye ndiye kaimu kiongozi wa shughuli za serikali bungeni leo Prof Mark Mwandosya ameliambia bunge asuhuhi ya leo kuwa serikali imefikia uamuzi huo kutokana na maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii iliyotaka muswada huo uondolewe ili wadau wapate nafasi ya kutoa maoni yao. Prof. Mwandosya amesema muswada huo utawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano ujao wa bunge ambao utakuwa ni wa bunge la 11 chini ya serikali ya awamu ya tano.

TOA MAONI YAKO JUU YA JAJI RAMADHANI KWENYE KITI CHA CHA URAISI

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi ya Katibu wa CCM wilaya ya Arusha alipofika kwaajili ya kupata wadhamini, Jaji Ramadhani ametaja sifa zingine kuwa ni pamoja na kuwa mwanachama wa CCM. Amesema ya sifa ya tatu kuwa anatakiwa kuwa mtu wa maamuzi sahihi na jasiri wa kufanya maamuzi hayo kwa kuwa wakati mwingine yanahusu watu wa karibu na marafiki lakini pia lazima rais awe na uzoefu katika uongozi, mtenda haki na mchapakazi. Amesema binafsi hana doa lolote litakalomfanya akose nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania na kwamba amekuwa na uzoefu wa kutosha ndio maana ameshawisisha kuomba nafasi hiyo ili aweze kuwatumikia watanzania. Aidha amesema kazi ya urais ni ngumu kuliko unavyofikiria, ilinichukua muda mrefu kufikiria kuomba nafasihiyo, lakini aliona anafaa kwa kuwa akiangalia uzoefu wake, hakuna shaka yoyote. Alipotakiwa kuzungumzia mgogoro wa muungano, Jaji Ramadhani amesema suala hilo liko wazi na kwamba muungano umekuwa na kero nyingi tangu nchi mwanzo na kudai atakapo chaguliwa kuwa Rais atahakikisha anabainisha kero husika na kuzifanyia kazi.

TANGAZA NASI KUPITIA BLOG YETU PENDWA YA MAUTUNDU SUPPLYER

CAR FOR SALE Toyota wist ‪#‎iko‬ katika hali nzuri Manufacturing : 2005 Cc1780 ‪#‎motor‬ vehicle Na road licence vimelipwa mpaka April 2016. Price: 9 Million fixed price. Inapatikana Dar es salaam Contact +255 759 607700, +255 683 024376