Tuesday, February 12, 2013

MTOTO WA AJABU AZALIWA IRINGA@SAMAHANI KWA PICHA







Uzito wa kichwa cha Zawadi ni kg 4 na nusu


Mtoto zawadi akiwa kapumzika kwenye kitanda





Wazazi wa mtoto Zawadi Gofrey Mwingune Bw Godfrey Mwingune (30) na mama wa mtoto huyo Mathar Kitago (28) wakimtazama mtoto wao kwa huzuni mwingi kutokana na kukosa fedha za matibabu kwa ajili ya kumsafirisha mtoto huyo kwenda kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa

HUJAFA hujaumbika ,Mungu ana makusudi yake ni yeye ni muweza wa yote kwani ndie aliyeumba mbingu na nchi pamoja na viumbe wote wasioonekana na wanaoonekana hivyo mwacheni Mungu aitwe Mungu,ni kauli ya wazazi wa mtoto Zawadi Godfrey Mwingune aliyezaliwa akiwa na macho matatu na kichwa mfano wa uyoga.

Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mama mzazi wa mtoto Zawadi Bi .Mathar Kitago (28) mzaliwa wa kijiji cha Kidegembye Lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe alisema kuwa hadi sasa anamwachia Mungu ambae ndie amempa zawadi ya mtoto huyo.

Kwani amesema kuwa ilikuwa ni siku ya jumapili January 13 mwaka huu aliposhikwa na uchungu na kukimbizwa katika kituo cha afya cha Kidegembye ambako alichukuliwa na kukimbizwa Hospitali ya wilaya ya Njombe Kibena kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo alisema baada ya kufika katika Hospitali hiyo aliingizwa katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa upasuaji na kubahatika kupata mtoto huyo japo kwa upande wake aliogopa sana baada ya kuonyeshwa mtoto huyo ila alipiga moyo konde kwa kuwa ni damu yake .

Bi Mathar mwenye idadi ya watoto watatu sasa akiwemo Zawadi anasema kuwa mtoto wa kwanza wa kiume ana miaka 9 na mtoto wa pili ni wa kike ana miaka 4 na wote alijifungua vizuri bila kufanyiwa upasuaji kama ilivyotokea kwa mtoto Zawadi.

Baba wa mtoto huyo Bw Godfrey Mwingune ambae anategemea kuendesha maisha yake kwa kilimo anasema kuwa yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Ikengeza Isimani na kuwa baada ya kupata mtoto huyo wa ajabu aliamua kurejea nyumbani kwa wazazi wake Igengeza Ismani ili kuwaonyesha mtoto huyo japo anatambua kuwa mtoto huyo ni zawadi kutoka kwa Mungu na ndio sababu ya kumpata jina la Zawadi pia.

" Kweli nilipomleta kwa wazazi kijijini nao wamebaki wakishangaa kuona mtoto wa ajabu hivyo ila sasa tunafanyaje yote ni mipango ya Mungu "

Mwingune alisema kuwa hali ya afya ya mtoto huyo si nzuri kwani mbali ya kuzawali wa kilo 4 na nusu ila bado anatatizo la uvimbe katika paji lake la uso pia kichwani kuna kovu kubwa ambalo ni kama ncha mbili hivi ambalo linatoa usaa mwingi na kuwa jeraha hilo alizaliwa nalo mbali na vituko hivyo pia alisema katika jicho lake la kushoto kwa juu kuna jicho la pili na kufanya mtoto huyo kuwa na macho matatu .

Alisema kuwa tayari mtoto huyo amepata kutibiwa Hospitali ya Kibena Njombe na Hospitali ya Rufaa Mbeya ila imeshindikana na madaktari wamemtaka amkimbize katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi ama nje ya Tanzania .

Hata hivyo mzazi huyo anasema kuwa kwa sasa pesa ya haraka inayohitajika ni kiasi cha Tsh. milioni 1.5 ili kumwezesha kwenda kuanza matibabu Muhimbili japo gharama za matibabu zinaweza kuongezeka zaidi wakati kwa upande wake hana uwezo wa kupata hata shilingi 100,000 na kuwapongeza wakazi wa Isimani ambao wamemchangia kiasi cha shilingi 300,000.

Mtandao huu wa www.mautundusupplyer.blogspot.com unakuomba wewe mdau na msamaria mwema popote pale duniani iwapo umeguswa na upo tayari kumsaidia chochote mtoto Zawadi ili kuokoa maisha yake kuweza kujitokeza kuchangia chochote kwa namba ya M-PESA 0754 026 299 au TIGO PESA 0712 750 199

No comments:

Post a Comment