Sunday, February 3, 2013

VIONGOZI NA WANACHAMA WA CHADEMA WAJIUNGA NA NCCR MAGEUZI

Viongozi waandamizi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,pamoja na wanachama 15 wa cha hicho,wanatarajia kujiunga na chama cha NCCR Mageuzi kesho kwenye Hotel ya Double J jijini Mbeya.Viongozi wa CHADEMA wanatarajia kukutana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya NCCR Mageuzi na mshauri wa mambo ya kisiasa Danda Juju ambae atamwakilisha mwenyekiti wa chama hicho Bwana James MbatiaJuju ambae ameshawasili jijini Mbeya kwa ajili ya kuwaapisha viongozi hao wa CHADEMA,kutokana na lengo kua ni kusambaratisha chama hicho.Viongozi hao ambao wanatarajiwa kujiunga na chama cha NCCR Mageuzi ni pamoja na aliekua katibu mkuu wa mkoa CHADEMA  Bwana Eddo Makata,aliekua mwenyekiti wa Baraza la vijana CHADEMA{BAVICHA} Bi.Juliana Shonza na aliewahi kugombea ubunge mbozi mashariki ndugu Mtera Mwampamba

No comments:

Post a Comment