Friday, February 15, 2013

GOLDIE HARVEY AFARIKI DUNIA.

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Goldie Harvey amefariki Dunia jana kwenye hospitali ya Reddington huko Victoria Island,Lagos.
Goldie Harvey.



Taarifa hizo zimethibitishwa kupitia akaunti zake za facebook pamoja na twitter ambazo alikua akizitumia,http://www.twitter.com/goldieharvey na pia http://www.facebook.com/goldieonline

Goldie amekutwa na umauti huo mara baada ya kutua kwenye mji wa Lagos kutokea nchini Marekani kwenye Tuzo za Grammy
Goldie akiwa na tiketi za Grammy.

Chanzo cha kifo chake hakijajulikana mpaka sasa kutokana na pia kuna muingiliano wa mawazo ambao bado unawachanganya watu kutokana kwamba huenda msanii huyu hajafa kutokana kwamba akaunti zake za kwenye mitandao ya kijamii kutumika mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment