Friday, February 22, 2013

ASKOFU AFICHUA SIRI NZITO BAADA YA MAUWAJI YA PADRI ZANZIBAR Na .Said Ng'amilo Iringa. ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi yaIringa, Dk. Odernbarg Mdegela, ametoboa siri nzito kuhusu uhalifu unaoendelea nchini, yakiwemo mauaji ya viongozi wa kidini na uharibifu wa nyumba za ibada, kwamba upo nyuma ya vikundi kadhaa vilivyopatiwamafunzo maalumu nje ya nchi kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo. Ingawa hakuvitaja moja kwa moja vikundi hivyo vinavyofadhiliwa ilikutekeleza mkakati huo, Askofu Mdegela amedai kwamba vikundi hivyo,vimepata mafunzo hayo na kwamba lengo ni kukamilisha mkakati huo. Kufuatia hali hiyo, Mdegela amewaandikia waraka, wanachama wote waJumuiya ya Makanisa ya Kikristo nchini (CCT) kuanza mara moja mfungowa saa 24 kuanzia leo (Maombi ya mnyororo), kusali dhidi ya uhalifuhuo kwa minajili ya kuwasaidia makachero kutoka ndani na nje ya nchikuwabaini wanaotekeleza mkakatihuo. Dk. Mdegela alitoboa siri hiyo leo wakati akizungumza na Waaandishiwa Habari katika kanisa kuu la kkkt lililopo eneo la Miyomboni sokoni Manispaa ya Iringa. ”Vikundi hivyo vinataka kuichafua serikali,kuuvunja muungano na kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kidini. Serikali ichukue au isichukue hatua, sisi tunakwenda madhabahuni na ndio maana nimeitisha maombi kwa makanisa yote ambayo ni wanachama wa CCT, ...Ingawa matamko haya, hayawezi kumaliza tatizo isipokuwa tutasugua goti ili kudhihirisha nguvu ya maombi,”Alisema Mdegela aliyekuwa ameongozana na wachungaji na baadhi ya wakuu wa majimbo ya KKKT. Kuhusu usalama wa makanisa yaliyopo chini ya KKKT na CCT, Askofu Mdegela ameagiza kila kanisa liimarishe ulinzi kila kona kutokana na mkakati unaotekelezwa kwa kificho na vikundi vinavyoshukiwa. ”Naagiza wekeni ulinzi kuanzia geti la mbele, la nyuma na kwenye kengele ili wakitokea watu hao, walinzi wapige kengele na kupambana nao. Huu ni wakati wa wakristo wote nchini kuingia na kuzama katika maombi ya mnyonyoro kuomba amani na kuepusha vurugu za kidini zinazoendelea nchini hivi sasa,”Alionya askofu huyo. Alifafanua kuwa vurugu hizo, zinatokana na baadhi ya vikundi vya kidini ambavyo amedai kwamba vinafadhiliwa na nchi zenye msimamo mkali kutaka kuueneza dini mojawapo kwa nguvu bila kufuata utaratibu na sheria za uenezaji. Askofu Mdegela amewataka wakristo kwa muda uliopo kuutumia katika maombi na kutojiingiza katika kuonesha tofauti za ukristo bali ni wakati wa kuungana kwa pamoja na kuingia katika maombi kwa kipindi chote kwa ajili ya amani na utulivu. Aliyataja matukio ya kuuawa kwa Mchungaji wa Kanisa wa kanisa la kiroho katika mkoa mpya wa Geita,kuuawa kwa Padri Evarist Mushi,kushambuliwa kwa risasi mwilini kwa Paroko Ambrose Mkenda,uchomaji moto nyumba za ibada na uharibifu wa mali za makanisa kadhaa nchini ni matokeo ya mkakati huo. "Kanisa limeingia katika mateso na tumesema hatutalipiza isipokuwa tunakwenda madhabahuni na kupiga tukiomba maombi ya mnyororo na tutashinda,"Alisisitiza Mdegela. wanataka nchiyetu isitawalike tuwekama nchi zisizo na amani duniani. Tunaimani umojaninguvu utenganoniudhaifu. Askofu Dkt Mdegela

No comments:

Post a Comment