Thursday, July 7, 2016

PASSPORT ITAKAYOTUMIKA KUSAFIRIA NCHI ZA AFRICA YAZINDULIWA AFRIKA MASHARIKI.

Viongozi wa umoja wa nchi za Afrikakwenye vikao vyake umepanga kutambulisha matumizi ya passport moja tu itakayotumika katika nchi zote zaAfrika ili kurahisisha safari za ndani yaAfrika. Passport hiyo ya kielekroniki imepangwa kuzinduliwa wiki ijayo Kigali Rwanda.
Hii imekuwa ni mpango wa muda mrefu kuwa na passport moja katika bara la Afrika ifikapo mwaka 2020 ambapo ambapo utarahisisha kusafiri kwa waafrika wote bilioni 1.1  katika nchi zote 55 zaa bara la Afrika.
Mwenyekiti wa Tume ya umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma amesema mpango huo una lengo la kujenga umoja wa Afrika na kurahisisha safari za ndani na kuwezesha uhuru wa usafirishaji wa  bidhaa na huduma ndani ya bara la Afrika

No comments:

Post a Comment