Wednesday, July 1, 2015

Matumizi ya gongo Rombo yapungua kwa 92% - DC

Unywaji wa pombe haramu ya gongo na ambazo hazina viwango umepungua kwa asilimiaa 92 wilayani Rombo baada ya serikali kukamata zana mbalimbali zinazotumika kutengezea pombe hiyo
Baadhi ya wanawake wa wilaya ya Rombo wakiandamana kuelekea kwa mkuu wa wilaya kama ishara ya kuunga mkono juhudi za serikali kupambana na matumizi ya gongo
Unywaji wa pombe haramu ya gongo na ambazo hazina viwango umepungua kwa asilimiaa 92 wilayani Rombo baada ya serikali kukamata mitambo 178, mapipa 3,500 ya malighafi, lita 550 za gongo, lita 108,000 za sumu za viwanda vya wazalishaji wakubwa wa pombe hizo kwa miezi mitatu iuliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembrise Kipuyo ametoa taarifa hiyo kwa mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo aliyepokea matembezi ya amani ya kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na upikaji na unywaji wa pombe hizo ambao unaathiri nguvu kazi yaliyoandaliwa na wanawake wa wilaya ya rombo...
Hata hivyo bw kipuyo ambaye anaongoza mapambano hayo baada ya kuhamia wilaya hiyo amesema, matembezi hayo yamempa nguvu na kasi mpya ya kupambana na wapikaji wakubwa wa pombe hizo ambao 58 kati yao wamekamatwa na kesi zao zinazoendelea mahakamani na wengine wamefungwa.
Katika taarifa yao wanawake hao wamewalaani baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaohamasisha unywaji na upikaji wa pombe hizo kwa kuiomba serikali ihalalishe gongo na kumtaka mkuu huyo wa wilaya asikatishwe tamaa na viongozi wa aina hiyo ambao ni wapinzani wa maendeleo.
Akipokea matembezi hayo ya kilomita mbili mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Wilbard Ringia amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ili kurejesha heshima ya kujieletea maendeleo kwa kufanya kazi kwa bidii ambayo imetoweka kutokana na unywaji wa pombe hizo.

chanzo EATV.


No comments:

Post a Comment