Friday, February 22, 2013

ELIZABETH MICHAEL "LULU" AJIANDAA TENA KURUDI SHULE SIKU CHACHE BAADA ya kupata dhamana msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ajipanga kujiendeleza Kimasomo ili aweza kupambana na changamoto za maisha. Akizungumza na mtadao huu msanii wa filamu ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu familia ya Lulu Mahfudh Hussein 'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake Alisema kuwa ingawa familia ina mikakati hiyo suala kubwa linalokwamisha kwa sasa ni kipato kwani familia yake haina uwezo wa kumlipia msanii huyo na badala yake anatakiwa Lulu kuanza kufanya kazi ili aweze kujikwamua kwa hilo Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa kutokana na kipato cha familia ya msanii huyo hivyo anatakiwa kwa sasa aweze kufanya kazi ya filamu ili aweze kujimudu kama ilivyokuwa mwanzo na maisha yaendele "Hapo awali alikuwa na uwezo wa kuidumia familia yake kwa njia ya kazi zake alikuwa anamsomesha mdogo wake wa mwisho pamoja na kulipa kodi ya nyumba alikuwa akifanya mammbo mengi hivyo na swala la kusoma lijukumu lake pia" alisema Mbali na hayo msanii Cheni alieleza kuwa Lulu yupo tayari kurudi shule ili aweze kujikwamua kielimu aweze kupambana na maisha hivyo jambo la msingi ni yeye kufikisha malengo yake aliyojipangia kwani umri wake bado ni mdogo na ananafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake Akizungumzia kwa upande wa kazi Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa endapo Lulu akimuomba amsimamie kazi zake atafanya hivyo kwani yote ni katika nia njema ya kumfikisha msanii huyo katika malengo aliyojipangia

at Wednesday, February 20, 2013 WATAHINIWA KIDATO CHA NNE WACHORA KATUNI KATIKA KARATASI ZA KUJIBIA MTIHANI Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi Fredy Azzah, Joyce Mmasi WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa. Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo fleva). “Mwaka jana tulikutana na ‘single’ yaani waliandika mashairi kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu, wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima kumlalamikia mpenzi wake. Miongoni mwa yaliyoandikwa ni mpenzi, umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…” alisema Dk Ndalichako. Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine waliandika malalamiko dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge. “Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…” alisema. Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya. Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao waliviita Messi (Lionel, mchezaji wa Barcelona) na zombi (ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa kwenye televisheni. Sababu za kufeli Dk Ndalichako alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya kwa nini matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya, lakini akadokeza kuwa huenda yametokana na wanafunzi wengi kukosa maarifa. Anasema mbali na waliojaza matusi na michoro, wanafunzi wengine waliofanya vibaya ni wale ambao hawakujaza chochote kwenye karatasi zao za majibu. “Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza.” Dk Ndalichako alisema kwa ku mbukumbu zake, hakuna matokeo mabaya kama ilivyo kwa mwaka huu yaliyowahi kutokea. “Tukiangalia tu kuanzia 2000, hakujawahi kutokea matokeo mabaya kama haya, kwa kweli hali haipendezi. Hata kabla ya kuyatangaza nilikuwa nayaangalia mara tatu tatu, sikuyapenda na inasikitisha kwa kweli,” alisema Dk Ndalichako. Chanzo: Mwananchi

ASKOFU AFICHUA SIRI NZITO BAADA YA MAUWAJI YA PADRI ZANZIBAR Na .Said Ng'amilo Iringa. ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi yaIringa, Dk. Odernbarg Mdegela, ametoboa siri nzito kuhusu uhalifu unaoendelea nchini, yakiwemo mauaji ya viongozi wa kidini na uharibifu wa nyumba za ibada, kwamba upo nyuma ya vikundi kadhaa vilivyopatiwamafunzo maalumu nje ya nchi kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo. Ingawa hakuvitaja moja kwa moja vikundi hivyo vinavyofadhiliwa ilikutekeleza mkakati huo, Askofu Mdegela amedai kwamba vikundi hivyo,vimepata mafunzo hayo na kwamba lengo ni kukamilisha mkakati huo. Kufuatia hali hiyo, Mdegela amewaandikia waraka, wanachama wote waJumuiya ya Makanisa ya Kikristo nchini (CCT) kuanza mara moja mfungowa saa 24 kuanzia leo (Maombi ya mnyororo), kusali dhidi ya uhalifuhuo kwa minajili ya kuwasaidia makachero kutoka ndani na nje ya nchikuwabaini wanaotekeleza mkakatihuo. Dk. Mdegela alitoboa siri hiyo leo wakati akizungumza na Waaandishiwa Habari katika kanisa kuu la kkkt lililopo eneo la Miyomboni sokoni Manispaa ya Iringa. ”Vikundi hivyo vinataka kuichafua serikali,kuuvunja muungano na kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kidini. Serikali ichukue au isichukue hatua, sisi tunakwenda madhabahuni na ndio maana nimeitisha maombi kwa makanisa yote ambayo ni wanachama wa CCT, ...Ingawa matamko haya, hayawezi kumaliza tatizo isipokuwa tutasugua goti ili kudhihirisha nguvu ya maombi,”Alisema Mdegela aliyekuwa ameongozana na wachungaji na baadhi ya wakuu wa majimbo ya KKKT. Kuhusu usalama wa makanisa yaliyopo chini ya KKKT na CCT, Askofu Mdegela ameagiza kila kanisa liimarishe ulinzi kila kona kutokana na mkakati unaotekelezwa kwa kificho na vikundi vinavyoshukiwa. ”Naagiza wekeni ulinzi kuanzia geti la mbele, la nyuma na kwenye kengele ili wakitokea watu hao, walinzi wapige kengele na kupambana nao. Huu ni wakati wa wakristo wote nchini kuingia na kuzama katika maombi ya mnyonyoro kuomba amani na kuepusha vurugu za kidini zinazoendelea nchini hivi sasa,”Alionya askofu huyo. Alifafanua kuwa vurugu hizo, zinatokana na baadhi ya vikundi vya kidini ambavyo amedai kwamba vinafadhiliwa na nchi zenye msimamo mkali kutaka kuueneza dini mojawapo kwa nguvu bila kufuata utaratibu na sheria za uenezaji. Askofu Mdegela amewataka wakristo kwa muda uliopo kuutumia katika maombi na kutojiingiza katika kuonesha tofauti za ukristo bali ni wakati wa kuungana kwa pamoja na kuingia katika maombi kwa kipindi chote kwa ajili ya amani na utulivu. Aliyataja matukio ya kuuawa kwa Mchungaji wa Kanisa wa kanisa la kiroho katika mkoa mpya wa Geita,kuuawa kwa Padri Evarist Mushi,kushambuliwa kwa risasi mwilini kwa Paroko Ambrose Mkenda,uchomaji moto nyumba za ibada na uharibifu wa mali za makanisa kadhaa nchini ni matokeo ya mkakati huo. "Kanisa limeingia katika mateso na tumesema hatutalipiza isipokuwa tunakwenda madhabahuni na kupiga tukiomba maombi ya mnyororo na tutashinda,"Alisisitiza Mdegela. wanataka nchiyetu isitawalike tuwekama nchi zisizo na amani duniani. Tunaimani umojaninguvu utenganoniudhaifu. Askofu Dkt Mdegela