Saturday, February 2, 2013

GARI LA MAREHEMU SHARO MILLIONEA LAUZWA.

Mama mzazi wa aliekua msanii wa muziki na filamu hapa nchini marehemu Hussein Ramadhani Mkiety alimaarufu sharo millionea.ameibuka na swala hili mara baada ya arobaini ya marehemu mwanae sharo na kusema kua analiuza gari la mwanae aliloliacha kutokana kwamba hawezi kuliendesha na pia haliwezi kukaa tu bila kufanya kitu hivo basi ameongeza kua hamtambui mwanadada aliejulikana kwa jina la Mary Lucas wa sumbawanga kua ana ujauzito wa marehemu sharo kutokana kwamba enzi za uhai wa mwanae sharo hajawahi kutambulishwa kua ana mpenzi au mchumba hivo huyu dada mimi simtambui.Alimaliza kwa kusema ivo.
Imeripotiwa na Gladness Mallya.

No comments:

Post a Comment