Monday, February 4, 2013

CHUPI ZABEBA MADAWA YA KULEVYWA MAREKANI.

Wanawake wawili toka nchini Marekani wamekamatwa na maofisa wa usalama nchini humo mara baada ya akina mama hao kupekuliwa na kukutwa na madawa ya kulevywa aina ya cocaine yenye thamani ya paundi milioni 2.Wanawake hao wamekamatwa yakiwa yamewekwa kwenye nguo za ndani za akina mama hao wakiwa wamezivalia ila zikiwa ni za bandia.
Pena Prisila na Michelle Blasingale walisimamishwa na maofisa wa Forodha kwenye uwanja wa ndege wa JFK baada ya kutoka Jamuhuri ya Dominika.Maafisa hao baada ya kuwakagua kwenye mizigo yao hawakuweza kuona chochote zaidi walipowakagua kwenye mavazi yao ndipo wakagundua kua walikua wamebeba madawa hayo huku kila mmoja akiwa na madawa zaidi kilo 3.Wanawake hawa wote kutoka Marekani wameweza kufunguliwa mashtaka ila Pena yuko nje kwa dhamana ila mwenzie Michelle yuko rumande.hivi ndivo ilivokua katika picha
nguo za ndani ndivo zilikua kwenye hali hii.




No comments:

Post a Comment