Thursday, January 31, 2013

TCRA YASHUSHA GHARAMA ZA KUPIGA SIMU





Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania {TCRA},imetangaza viwango vipya ambavyo makampuni ya simu simu za mikononi yanatakiwa kuwatoza wateja wao pindi wafanyapo mawasiliano kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kwa gharama nafuu zaidi.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa TCRA John Nkoma kua makampuni hayo yanatakiwa kushusha gharama zao kutoka shilingi 113 kwa dakika mpaka kufikia shilingi 34 na senti 92 kwa dakika na ameendelea kusema hayo yote yamechangiwa na kupanda kwa maisha.Ametoa agizo hilo hivi karibuni akiwa anazungumza na waandishi wa habari juu ya kufika taarifa   kwa umma na akasema kua utekelezaji huu wa gharama za kupiga simu kwa shilingi 34 na senti 92 utaanza tarehe moja mwezi machi na endapo kampuni yoyote itaenda kinyume na sheria hio basi hatua sitahiki zitachukuliwa

No comments:

Post a Comment