Leo kwenye Hekaheka ya @CloudsFM alikuwepo Ally Nipishe,
moja ya jamaa ambao waliwahi kufanya poa kwenye Bongo Fleva alafu
baadae akawa kimya hivi, viko vingi vilitokea katikati na sisi hatukujua
kuhusu hilo, leo ametoa majibu yote.
Staa mwingine aliyekuwepo ni Pipi, jina lake liko kwenye list ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri pia kwenye Muziki TZ… Ally kasimulia
vingi ikiwepo ishu ya mikasa mbalimbali iliyomkuta, kuna wakati
alikamatwa akafungwa jela baada ya kuhusishwa na wizi wa pesa.
Ishu ilianzia pale alipouziwa gari,
kumbe lilikuwa ni gari ambalo liliibiwa na ndani yake kulikuwa na pesa
pia.. mpenzi wake alihusika pia kumuunganisha na waliomuuzia gari hilo.
Pipi naye
amezungumzia mambo mengi, kumbe yeye na mpenzi wake wanatumia simu
moja… yeye na mume wake wana misingi mizuri ya uaminifu, hawana mambo
mengi kwa hiyo hawana sababu ya kufichana.
Nimekusogezea sauti yao hapa chini, bonyeza play kuisikiliza.
Chanzo,Millard Ayo.
Chanzo,Millard Ayo.
No comments:
Post a Comment