Wednesday, July 1, 2015

MKE AZUILIWA KWENDA KUMZIKA MUME WAKE,KISA KIKO HAPA

Hekaheka ya leo inatokea Shinyanga ambapo wanafamilia pamoja na majirani walimzuia mke wa marehemu kwenda kumzika mume wake kwa madai kuwa alikua akimnyanyasa enzi za uhai wake.
Wakati mume wake anafariki mama huyo hakuwepo na alipopigiwa simu kuwa mume wake amefariki alirudi nyumbani na kuwakuta ndugu wa mume wake na majirani wakiomboleza lakini yeye akionekana kutojali na macho yakiwa makavu na hakuwa na dalili ya huzuni.
Majirani wanasema aliwahi kumkana mume wake tangu zamani pamoja na kumtesa huku akiishi na mume mwingine ambaye ni mume wa mtu ndani ya nyumba ya mume wake huyo.
Wanandugu wa mume wakishirikiana na majirani na Mwenyekiti wa mtaa walimshusha kwenye gari mama huyo na watoto wake wakati wakienda kuzika kijijini kwao Bukoba na kuwaacha wenyewe.Chanzo clous fm.

No comments:

Post a Comment