Saturday, July 4, 2015

Aliripoti Polisi baada ya kutishiwa maisha na mchumba wake-Shamsa












Muigizaji wa filamu Shamsa Ford amefunguka na kusema kwamba tangu aachane na Ex boyfriend wake Dickson Matoke aliwahi kuwatishia kuwauwa yeye na mwanae zaidi ya mara 10.
Akizungumza na millardayo.com alisema…’Ni kweli wakati nilipokuwa katika mahusiano naye alikuwa ni mtu ambaye anapenda sana kuniambia neno nitakuuwa mimi na mwanangu ndio maana nilikuwa naogopa sana kwasababu nilihisi kuwa anaweza kufanya lolote kunikomoa na nilienda hadi polisi kuchukua RB yake ili kama lolote litakalotokea basi yeye atakuwa amehusika, yaani yule alikuwa ananiambia kabia yuko serious mbaya kuwa ataniuwa mimi na mtoto wangu lisha kwangu alikuwa anawaambia hata marafiki zangu ni mashahidi na mbaya zaidi alikuwa anasema hayo maneno na mbaya zaidi alikuwa anawaambia hata ndugu zake.
 
Shamsa akiwa na ex-boyfriend wake 
 Hayo maneno alikuwa anayaongea wakati bado niko naye kwenye uhusiano lakini ndio hivyo malumbano malumbano na mimi nilikuwa nimeshachoka na hizo tabia zake lakini baada ya kuachana naye ni vitisho labda anataka kumuona mtoto anatumia vitisho mara sasa ninapomnyima mtoto basi anatumia vitisho basi mimi nikikumbuka lile neon lake la kusema ataniuwa basi moyoni sina amani….’alisema

No comments:

Post a Comment