Friday, June 26, 2015

MUSWADA WA HABARI WAONDOLEWA BUNGENI

Serikali imeuondoa muswaada wa sheria ya haki ya kupata habari uliokuwa uwasilisilishwe na kujadiliwa katika mkutano unaondelea wa bunge mjini Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na wizara maalum ambaye ndiye kaimu kiongozi wa shughuli za serikali bungeni leo Prof Mark Mwandosya ameliambia bunge asuhuhi ya leo kuwa serikali imefikia uamuzi huo kutokana na maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii iliyotaka muswada huo uondolewe ili wadau wapate nafasi ya kutoa maoni yao. Prof. Mwandosya amesema muswada huo utawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano ujao wa bunge ambao utakuwa ni wa bunge la 11 chini ya serikali ya awamu ya tano.

No comments:

Post a Comment