Tuesday, November 12, 2013

TONYA BUSINESS AAIBIKA,SOMA HII

Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto ya jiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu pamoja na gari yake.



Mwanamuziki huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta Jijini Dar pamoja masista du wakila bata ghafra kundi la watu watano lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.

Habari zaidi toka kwa chanzo chetu kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu


No comments:

Post a Comment