Sunday, March 17, 2013

HATA YA PAGE YAKO YA FACEBOOK BAADA YA KIFO NI NINI,SOMA HAPA.

Habari na Dr.Paul Masua
Hujafa hujaumbika. Kifo ndio hatma ya uhai. Kuna mambo mengi binadamu anaweza kuepuka.Lakini si kifo. Hata usipofariki kwa maradhi au ajali;umri je? Kifo ni sheria.

Dini zinatufundisha kujiandaa kiroho.Tuwe tayari. Maana kifo hakina saa wala dakika.Kifo hakibagui. Tajiri au maskani,kijana au mzee,mcha Mungu au mdhambi wote hatma yao ni moja. Kifo. Usipokufa leo,utakufa kesho.
Facebook.  Kwa sasa mtandao huu wa kijamii unawatumiaji zaidi ya bilioni moja duniani kote. Watu wa rika,nyadhifa,uwezo,elimu na dini mbalimbali wanatumia Facebook. Idadi hii ikiongozwa na vijana na watu wenye umri wa kati. Hawa ndio wapenzi zaidi wa facebook.
Wapendwa wetu wako wapi. Baadhi  ya ndugu,jamaa na marafiki waliokuwa wanatumia facebook leo hawapo. Wamefariki. Hatutawaona tena. Kuna wengine tuliwasiliana nao kupitia facebook,wengine waliacha ujumbe. Wengine maneno ya huzuni. Tena  masaa machache kabla ya vifo vyao. Hakika tunawakumbuka. Tunawaombea wapumzike kwa amani.
Mara chache watumiaji wa facebook huweza kuchangia maneno yao ya siri na watu wengine. Hivyo baada ya kifo hakuna mtu mwingine anayeweza kutumia ukarasa ule wa facebook.
Kurasa zao za facebook ziko wazi. Zingine zinaendelea kutumika. Zingine zinatumika pasipo kihalali. Baadhi ya wadhalimu wanatumia kurasa hizo kuandika maneno ya kashifa na dhihaka. Dhihaka hata baada ya kifo. Hakika huu ni udhalimu.
Fikiria ni nini ufanye. Wosia. Unaweza kuweka neno lako la siri katika wosia? Je ni busara kurithisha neno lako la siri? Au unaweza kuchangia neno lako la siri na mama mzazi kama yupo hai.
Hata hivyo kufuatia kukua na kupanuka kwa mitandao ya kijamii ni vyema serikali kuweka sheria. Sheria zinazosimamia matumizi ya mitandao ya kijamii. Hii itasaidia kuondoa pengo lililopo. Hasa baada ya kifo cha mtumia

No comments:

Post a Comment