Tuesday, February 26, 2013

NAIBU WAZIRI WA MAJI HALI TETE Dr. Binilith Mahenge HALI TETE Hivi karibuni katika mkutano wake wa hadhara Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika (CHADEMA) amemuweka kwenye wakati mgumu Naibu waziri wa Maji Mh. Dr. Binilith Mahenge na waziri wake Mh. Profesa Jumanne Magembe. Dr. Mahenge amewekwa kwenye wakati mgumu kufuatia tendo la Mheshimiwa Mnyika kugawa namba ya Mh. Mahenge kwa wananchi ili wananchi wampigie Dr. Mahenge na kumuuliza ni lini yeye na waziri wa Maji watatekeleza ahadi yao ya kuhakikisha kero ya maji inaisha Dar es salaam. Namba za Dr. Mahenge za Tigo na Voda zilirushwa kavu kavu kwa wananchi. Kabla ya hapo wiki moja iliyiopita Prof. Magembe alifanya mkutano na wananchi wa Ubungo na kuwaahidi kuwa kero ya maji itakuwa imetatulika ifikapo tarehe 20 mwezi February. Lakini kwa mujibu wa taarifa za wananchi wa ubungo ni kuwa ahadi hiyo ilikuwa hewa. Mwaka jana kwenye kikao cha Bajeti, Bajeti ya wizara ya maji ni moja ya wizara ambazo bajeti zake zilipita kwa msukumo wa madam Spika, na Kikao cha bunge kilichopita Mh. Mnyika aliwakilisha hoja binafsi kuhusiana na kero za maji, Hoja ambayo iliondolewa baada ya kufanyiwa marekebisho

No comments:

Post a Comment