Monday, December 30, 2013

MOVIE YA MWISHO YA JET LI KABLA HAJAUGUA

Hiii ni movie aliyoitoa Jet Li mkali wa action movie kabla hajapatwa na ugonjwa unaomsumbua kwa sasa kiasi kwamba hawezi hata kupiga mazoezi madogo madogo

WAPENDA MOVIE HIII INAKUHUSU

Kwa wale wapendao movie hii ni kwa ajili yenu,RISE OF AN EMPIRE inatazamia kutoka mwaka ujao

SHULE YAFAULISHA WANAFUNZI WOTE KINGALI INA MWALIMU MMOJA TOKA CHEKECHEKEA MPAKA DARASA LA 7

Katika hali isiyo ya kawaida, shule moja wilayani Bagamoyo imekutwa ikiwa na mwalimu mmoja tu anayefundisha wanafunzi kuanzia chekechea hadi darasa la saba, wote wakifundishwa katika chumba kimoja kwa kutumia ubao mmoja. 

Hata hivyo, katika matokeo ya Darasa la Saba Mwaka huu, wanafunzi wote 12 walifaulu kuingia kidato cha kwanza.


Shule hiyo ya msingi Machala, iliyokuwa na idadi ya wanafunzi 198 na imejengwa kwa majani kuanzia chini hadi kwenye paa.

Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea shule hiyo, alimkuta mwalimu huyo akiwafundisha wanafunzi hao wa madarasa tofauti wakiwa kwenye chumba kimoja, huku ubao wa kufundishia ukiwa umechorwa mistari mitatu kutenganisha masomo ya chekechea hadi darasa la pili, mstari mwingine darasa la tatu hadi la tano na mwingine darasa la sita hadi la saba.


Mwalimu huyo, Christopher Rukutu, aliliambia NIPASHE Jumamosi kuwa shule hiyo hutumia kivuli cha mti kama ofisi.

Shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Mihunga Kata ya Miono, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, ilianzishwa na serikali tangu mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 12 ambao wamemaliza darasa la saba, mwaka huu na kubahatika kufaulu wote.

Kwa mujibu wa mwalimu Rukutu, wanafunzi wote waliofaulu walipata alama za A na B isipokuwa mmoja aliyepata alama C. 

Pamoja na kuwa katika mazingira magumu, shule hiyo kiwilaya ilishika nafasi ya sita na kimkoa nafasi ya 20.

Alisema shule hiyo haina vitabu vya kiada wala vya kufundishia na amekuwa akiazima kutoka shule za jirani.

“Ninafundisha kwa akili za kuzaliwa sina kitabu cha mtaala wa elimu, nguvu zangu zote nilimalizia kwa darasa la saba ili wajue kusoma, kuandika na kuhesabu.

Kwa mwaka mzima sijafundisha darasa la nne nina wasiwasi matokeo yao hayatakuwa mazuri kwa sababu niko peke yangu," alisema kwa masikitiko.

Alifafanua kuwa tangu shule hiyo ianzishwe, serikali ilikuwa imewapanga walimu wawili tu, ambao kutokana na mazingira kuwa magumu waliripoti bila kuingia darasani na kuaga baada ya kuonyesha vyeti vya hospitali vinavyonyesha kuwa afya zao haziwezi kustahimili mazingira magumu.

Aliilalamikia serikali kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya kwa kuisahau shule hiyo bila kuipa msaada wowote.

Mbali na kukosa msaada, shule hiyo pia inatumia tundu moja tu la choo kwa wanafunzi wa kike na kiume na kusababisha wengi wao kujisaidia vichakani.Alisema kutokana na hali hiyo, wanafunzi wengi hushambuliwa na ugonjwa wa kichocho.

Aliiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuwapangia wanafunzi wake 12 waliofaulu katika shule yake ya Machari kwenye shule za sekondari zenye mahitaji muhimu ili kuwapunguzia mateso wanafunzi hao.

Alisema wanafunzi wake hawajawahi kuona vitabu vya kujisomea na huduma muhimu za kiafya.

CHANZO: NIPASHE

HUU NDIO UTOFAUTI BAINA YA TAJIRI NA MASIKINI.

Maisha ya watu wenye kipato na wasio na kipato,kuna utofauti mkubwa sana hasa kwa wale wasio na kipato ndio wengi kuliko kwa walionacho kipato.
Hatupendi maisha haya ila tutafanyaje sasa wakati ndio AMANI ya moyo inapopatikana.

MAISHA NI MAPAMBANO,HAPANA KUCHOKA.

Kila mwananchi wa nchini au taifa lolote Duniani anahitaji kuishi katika mazingira mazuri ambayo yatamfanya awe na furaha na amani muda wote kutokana na mazingira anayoishi kwanza.Lakini kutokana na mambo mbali mbali ambayo aidha watu wamejisahau au jamii inayowazunguka kushindwa kuwakumbusha kwa kufanya mambo kadhaa nao wameshindwa kukumbuka wapi walipo.
Hii ni nyumba ambayo mtu anaishi na anaendeshea maisha yake hapa kwa muda mrefu sana.Sasa swala laja kuwa huyu mkazi anaekaaa katika mazingira haya anaweza kumsisitiza mtoto wake aweze kwenda shule ili aweze kumkomboa mzazi wake kutoka katika mazingira haya?.Pia ni wazazi wachache sana ambao wanauwezo huo kutokana na wengine huishi katika hali ngumu sana za kimaisha kiasi kwamba wengine wanauwezo wa kupata mlo wa mmoja kwa siku au siku zingine hamna kabisa.
Maisha ya sasa ni ya kupambana na sio ya kubweteka na kukaa vijiweni kutokana kwamba vijiwe hivyo hivyo huleta maandeleo na pia kupitia vijiwe hivyo hivyo pia huwapeleka vijana wengi katika mstari tofauti na ule ambao walikuepo awali.
Naamini kwa kupitia changamoto unazokutana nazo unaweza kufanya kitu ambacho kitakua tofauti na kupitia wewe unaweza kusababisha watu wengine wakatoka sehemu waliyokuwapo na kwenda sehemu nyingine.HAKUNA KINACHOSHINDIKANA CHINI YA JUA KAMA UNAJITAMBUA ANZA SASA.