Saturday, December 21, 2013

KAMA HUKUISOMA HII INAKUHUSU.BASI LA TAQWA LILIVONUSURIKA KUWAKA MOTO.

Basi la Taqwa lililokuwa na zaidi ya abiria 60 ambao wamenusurika kupoteza maisha yao baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kupitia mjini Ngara kueleke Jijini Bujumbura nchini Burundi kunusurika kuwaka moto wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Basi la abiria la Kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 964 BHS aina ya SCANIA likiwa limenusurika kuteketea juzi ( Desemba 18,2013) majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Mkajagali kijiji cha Kumuyange, nje kidogo ya mji wa Ngara.

UKATILI HUU MUME AMPIGA MKE WAKE WA NDOA NA KUMVUNJA TAYA.

Mariam Crispin Kilimba(52)mkazi wa Ipuli manispaa ya Tabora anayedaiwa kupigwa na mumewe Bw.Himid Hassan Kitebo(58)ambaye ni mganga wa Kienyeji na kusababisha kumvunja taya.


Bi.Joha Aman(38)mkazi wa kata ya Isevya alipigwa na mumewe na kujeruhiwa vibaya ambapo amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.Matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Tabora bado yanaendelea kushika kasi siku hadi siku.

"BAADA YA KUMVUA MADARA ZITTO, SASA NI ZAMU YA DK. SLAA KUTIMULIWA CHADEMA"....MWIGAMBA

chadema mkoa wa Arusha Samson Mwigamba amesema kuwa mpango unaofuata kwa sasa ni kumuondoa Dr slaa ndani ya chadema.

amesema baada ya zitto kuondolewa ndani ya chama mtu atayefuata katika kushughulikiwa ni Dr Slaa ambaye kwa sasa amekuwa amekuwa akifanya shughuli za chama kwa kupelekwa pelekwa bila yeye mwenyewe kujua.


Mwigamba amesema kuwa upo mkakati kabambe unaendeshwa na baadhi ya watu kwa kushirikiana na watu walio nje ya chama ili kukimaliza chama kabla ya kufika kwenye uchaguzi mkuu 2015.

Amesema kuwa Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambaye yupo karibu sana na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ndio vinara wa mkakati wa kukiangamiza chama, huku John mnyika na Tundu Lissu wakijiweka mbele bila kujua hatima yao.

MEYA NA FAMILIA YAKE WAPIGWA RISASI NA KUFARIKI WAKIWA UWANJA WA NDEGE..

6063 

Sasa hivi matukio ya watu kupigwa risasi kwenye mikasa ambayo sio ya kawaida sio Tanzania tu bali hata kwenye nchi nyingine au maeneo mengine ambayo hayakuwahi kuwa na rekodi za ukatili wa aina hii.

Taarifa ya leo inamuhusu Meya wa mji wa Labangan ambae amepigwa risasi akiwa na watu wengine watatu maeneo ya airport huko Manila Philippine ambapo Ukol Talumpa imeripotiwa alipigwa risasi pamoja na mke wake, mtoto wao wa miezi 18 na mtu mwingine mmoja na kufariki.

Ripoti hii inasema watu wengine wanne wamejeruhiwa kwenye tukio hilo wakati mshambuliaji huyo alipotekeleza shambulio hilo huku kiongozi huyo aliekuwa nje ya terminal 3 ya Airport akisubiri usafiri ambapo ndio mtu mmoja akiwa kwenye pikipiki alipita na kufyetua risasi kwa karibu na kukimbia na pikipiki yake.

Chanzo cha tukio hili bado hakijajulikana.
(hiyo picha ya juu inamuonyesha Ukol Talumpa mwenyewe)