Habari na Dr.Paul Masua
Hujafa hujaumbika. Kifo ndio hatma ya uhai. Kuna mambo mengi binadamu
anaweza kuepuka.Lakini si kifo. Hata usipofariki kwa maradhi au
ajali;umri je? Kifo ni sheria.
Dini zinatufundisha kujiandaa kiroho.Tuwe tayari. Maana kifo hakina saa
wala dakika.Kifo hakibagui. Tajiri au maskani,kijana au mzee,mcha Mungu
au mdhambi wote hatma yao ni moja. Kifo. Usipokufa leo,utakufa kesho.
Facebook. Kwa sasa mtandao huu wa kijamii unawatumiaji zaidi ya bilioni
moja duniani kote. Watu wa rika,nyadhifa,uwezo,elimu na dini mbalimbali
wanatumia Facebook. Idadi hii ikiongozwa na vijana na watu wenye umri
wa kati. Hawa ndio wapenzi zaidi wa facebook.
Wapendwa wetu wako wapi. Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki waliokuwa
wanatumia facebook leo hawapo. Wamefariki. Hatutawaona tena. Kuna
wengine tuliwasiliana nao kupitia facebook,wengine waliacha ujumbe.
Wengine maneno ya huzuni. Tena masaa machache kabla ya vifo vyao.
Hakika tunawakumbuka. Tunawaombea wapumzike kwa amani.
Mara chache watumiaji wa facebook huweza kuchangia maneno yao ya siri na
watu wengine. Hivyo baada ya kifo hakuna mtu mwingine anayeweza kutumia
ukarasa ule wa facebook.
Kurasa zao za facebook ziko wazi. Zingine zinaendelea kutumika. Zingine
zinatumika pasipo kihalali. Baadhi ya wadhalimu wanatumia kurasa hizo
kuandika maneno ya kashifa na dhihaka. Dhihaka hata baada ya kifo.
Hakika huu ni udhalimu.
Fikiria ni nini ufanye. Wosia. Unaweza kuweka neno lako la siri katika
wosia? Je ni busara kurithisha neno lako la siri? Au unaweza kuchangia
neno lako la siri na mama mzazi kama yupo hai.
Hata hivyo kufuatia kukua na kupanuka kwa mitandao ya kijamii ni vyema
serikali kuweka sheria. Sheria zinazosimamia matumizi ya mitandao ya
kijamii. Hii itasaidia kuondoa pengo lililopo. Hasa baada ya kifo cha
mtumia