Friday, February 15, 2013

MBUNGE SHAROBARO MIKE SONKO NDANI YA VAZI LA VALENTINE'S DAY.

The swaggalicious Politician kutoka Kenya Gideon Mbuvi k.p.a Mike Sonko alivoisheherekea siku ya wapendanao ''valentine's day'' na kuiweka Hammer yake kwenye staili yake kama hivi.



Wakati wa siku hii ya wapendanao,watu wengi wakionesha upendo wao kwa wale wawapendao aidha wapenzi,baba,mama,dada,kaka ama hata rafiki kikubwa na cha msingi ni kumuonesha upendo.Kwa ndugu Mike Songo aliweza kuitumia kwa kupiga kampani kwa ajili ya u-senetor wa jiji la Nairobi na kuamua kuwaonesha wapiga kura wake kua anawapenda sana na anahitaji kura zao sanaaaaaa.
Mike Sonko.

GOLDIE HARVEY AFARIKI DUNIA.

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Goldie Harvey amefariki Dunia jana kwenye hospitali ya Reddington huko Victoria Island,Lagos.
Goldie Harvey.



Taarifa hizo zimethibitishwa kupitia akaunti zake za facebook pamoja na twitter ambazo alikua akizitumia,http://www.twitter.com/goldieharvey na pia http://www.facebook.com/goldieonline

Goldie amekutwa na umauti huo mara baada ya kutua kwenye mji wa Lagos kutokea nchini Marekani kwenye Tuzo za Grammy
Goldie akiwa na tiketi za Grammy.

Chanzo cha kifo chake hakijajulikana mpaka sasa kutokana na pia kuna muingiliano wa mawazo ambao bado unawachanganya watu kutokana kwamba huenda msanii huyu hajafa kutokana kwamba akaunti zake za kwenye mitandao ya kijamii kutumika mpaka sasa.

M4C YAWAFIKIA WAGONJWA MWANANYAMALA.

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ,leo kimefanya maadhimisho ya siku ya wapendanao alimaarufu Valentine Day kwa kuwatembelea wagonjwa walioko kwenye hospital ya mwananyamala ilioko Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.Matembezi hayo yaliongozwa na Madiwani,viongozi na wanachama wa chama hicho.
Katika matembezi hayo waliweza kufanya usafi ikiwemo kufyeka,kufagia,kuchoma takataka moto na pia kupata changamoto wazipatazo wagonjwa pamoja na wauguzi.















wagonjwa waliogawiwa juice na maji pamoja na mikate kutoka kwa wanachama na viongozi wa CHADEMA.

wanachama wakiwa kwenye moja ya majukumu.

baadhi ya wauguzi waliokuepo zamu.













RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH.JAKAYA MRISHO KIKWETE AKITOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO NA KUSAINI KWENYE KITABU CHA MAOMBOLEZO,KWENYE MSIBA WA ASKOFU THOMAS O. LAIZAR.

Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete akitoa salamu zake za mwisho kwa askofu Thomas O. Laizar kwenye Dayosisi ya Kaskazini Kati la kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) leo,kwenye kanisa la KKKT Arusha mjini.
Raisi Jkaya Mrisho Kikwete akiwafariji wanafamilia ya marehemu Askofu Thomas O. Laizar
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akiandika kwenye kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizar. 
(Picha zote na Fredy wa Ikulu)