Monday, February 11, 2013

CHRISS NA RIHANNA TENA.

Haya tena wagombanao siku zote ndio wapendanao,huu ni usemi ulio kwenye lugha yetu ya kiswahili na kupitia usemi huu tunaweza kuona hapo nyuma kidogo ni ugomvi uliokuepo baina ya wapendanao hawa Chriss brown na Rihanna ambapo Rihanna aliweza kupigwa na Chriss na kumsababishia majeraha kadhaa kwenye uso wake hali iliyopelekea Chriss kufikishwa mahakamani na kufungiwa kuonana na mwanadashosti huyo.
Hivi karibuni waliweza kurudiana na kua kama awali na kuonesha mapenzi yao hadharani,haya yamejiri hapo jana kwenye tuzo za Grammy huko Marekani ambao wapendanao hawa walikua kwenye pozi mbali mbali kama zinavoonekana hapa chini kwenye picha za walimbwende hawa.
Chriss & Rihana










Thanks Sam Misago kwa picha hizi.






PAPA BENEDICT WA 16 AOMBA KUSTAAFU.

Papa Benedict wa 16 ameomba kustaafu mara baada ya hali yake kiafya kutokumudu shughuli za utendaji wake kua chini.Hayo yamesemwa na msemaji mkuu kutoka huko makao makuu ya kanisa hili kuwepo nchini Italia.
Benedict wa 16 ni miongoni mwa mapapa ambao waliowahi kuomba kustaafu wenyewe kutoka na sababu zilizo nje ya uwezo wao,papa huyu amekua wa pili kuomba kujiuzulu nyadhifa hio.Papa mwenye miaka 85 mpaka sasa ameweza kukaa na kutenda kazi zote za kipapa toka aprili 2005 mpaka hii leo ambapo kasema rasmi.

NGOMA YA P-UNIT WAKIWA NA SAUTI SOL SIKILIZA NA KUIDOWNLOAD HAPA.

Hii ndio ngoma walioitoa P-unit wakiwa na Sauti sol wote wakitoka Kenya.isikilize hapa na kui-download hapa. P Unit feat- Sauti Sol GENTLEMAN