Friday, February 8, 2013

VIDEO MPYA YA BARNABA,ITIZAME HAPA.

Hii ndo video mpya ya Barnaba boy kama hujapata fursa ya kuitazama iko hapa.


KAMA HAUJAUSIKIA WIMBO KIGOMA ALL STARS=NYUMBANI.SIKILIZA NA DOWNLOAD HAPA.

AMA ZAKE AMA ZANGU KWA ATAKAEMFANYIA LULU SHEREHE.

Msaniii wa filamu nchini Munah ,ameweza kuelezea kwamba yeyote ambae ambae anataka kumfanyia sherehe msanii mwenzake Elizabeth Michael alimaarufu LULU,yukoayari kwa lolote mara baada ya msanii huyo kurejea mtaani kwa dhamana.Na Munah kasema hayo baada ya kusikia kua kuna watu na wasanii wengine wanaotaka kumfanyia sherehe msanii huyo.Munah ambae amechangia kwa asilimia kubwa kwa mchango wake mpaka lulu kua nje kwa dhamana hio.
Wakati anaongea na Mautundu supplyer Munah alisema haya ''Ama zake au ama zangu kwa yule ambae anataka kumfanyia Lulu sherehe,maana alipokua segerea hawakupata muda wa kwenda kumuona ila leo yuko mtaani,eti wanataka kumfanyia  yao kwenda segerea ntaenda mimi.''Alisema Munah.
Munah.

LEO NDANI YA KAWE NA FM ACADEMIA.

Wazee wa ngwasuma kwa jina la bendi ni FmAcademia,leo wanategemea kutambulisha nyimbo zao kadhaa zilizomo kwenye album yao mpya inayojulikana kwa jina la ''chuki ya nini'',uzinduzi huu wa hizi nyimbo kadhaa utafanyika ndani ya ukumbi wa Masae view Garden uliopo ndani Kawe ambayo wanategemea kuizindua mapema mwaka huu.
Akiongea na Mautundu supplyer kwa njia ya simu,msemaji wa Fm academia bwana Kelvin Mkinga amesema kua leo wataachia silaha zao zote zilizoko kwenye album yao mpya ambao itakuja kutambulishwa hapo baadae.

Wanenguaji wa Fm academia.

PICHA GANI INAKUFURAHISHA HAPA.

picha namba 1.
picha namba 2.
picha namba 3.



BAADA YA KUNUSURIKA KUTEKETEA,MV BUKOBA YAENDELEA NA SAFARI YAKE.














safari yaanza kwenda bukoba.


abiria wakitafakari safari.


meli ikiondoka bandarini mwanza.

Magari yakipakiwa kwenye meli.

KIM KARDASHIAN KUBADILI JINA.

Kanye West amwambia mpenzi wake ambae pia ana ujauzito wake mwanadada Kim Kardashian abadili jina lake kutoka lilivokua Kim Krdashian na kuitwa Kim West,mara baada ya kuanza michakato ya kufunga pingu za maisha.
Kim aliweza kukubali kuchukua na kua analitumia jina hilo pia alitaka mwanao ambae nae Kim alidai aitwe ivo pia kwa mujibu wa jarida la Star.
Lakin Kim aliendelea kumwambia Kanye West kua hata nikiwa natumia jina lako bado ntabaki kua Kardishian,kauli hio ilimdhoofisha Rapa huyo na kumtaka Kim aifute kauli hio lakin aligoma kuifutaPia Kim aliamua kumwambia hivo Kanye ili pia atambue kua hayuko nae kwa kigezo cha pesa anazomiliki rapa huyo.

YAHYA TOURE AJA NA LAKE KWA MAN UNITED.

Mchezaji wa kimataifa wa Ivory coast na pia wa Manchester city Yahya Toure ailerejea kutoka kwenye mashindano ya kimataifa akiwa anaiwakilisha timu yake ya Ivory coast ambatu mwishoni mwa juma lililopita waliweza kutolewa na kwenye mashindano hayo na timu ya taifa ya Nigeria ambayo iliwafunga na kuwafanya miamba hao waweze kuaga mashindano hayo.
Mara baada ya kufika kwenye timu yake ya Manchester city Toure alisema haya kwa ajili ya wapinzani wao na wanaoshikilia ligi kuu ya Epl kua safari ya kunyakua kombe/taji la ligi hio bado mbali sana kwa kusema ivo basi nimekuja kuongeza nguvu kwenye kikosi changu na hivo kupunguza au kuondoa tofauti iliyokuwepo ya pointi 9 dhidi yao.