Monday, February 4, 2013

VALENTINE'S SPECIAL NA BEN POL & LINNAH

Ule usiku wa Valentine's Day uliokua unatazamiwa kua ni usiku wa wasanii Ben pol & Linnah ambao ulitakiwa kufanyika kwenye viwanja vya Jangwani Sea Breeze Alhamisi tarehe 14/02/2013 sasa itafanyika Nyumbani Lounge.
Waandaaji wa show hio,Keys Production  wameitaarifu Mautundu supplyer kwamba show hio imehamishiwa ''Nyumbani'' kutokana kwamba wanataka kila mpenda Burudani aweze kufika na kushuhudia kinachofanyika pale huku akiwa na Valentine wake ndani ya mng'aro.Aidha show wameiboresha baada ya kumuongeza Kassim Mganga na T.I.D.

MWANAMKE MFUPI NA MWANAUME MFUPI DUNIANI HAWA HAPA.

Kutoka nchini India mwanafunzi Joyti Amge ameweza kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia mara baada ya kujulikana kua yeye ndo mfupi kuliko wote kwa kuweza kua na urefu wa sentimeta 62.8 akiwa ameshika rekodi kwa upande wa wanawake na kwa wanaume nafasi hio iliweza kushikwa na Chandra Bahadur Dungy kutoka Nepal.Chandra mwenye miaka 72 ana urefu wa sentimeta 54.6
Chandra & Joyti.

CHUPI ZABEBA MADAWA YA KULEVYWA MAREKANI.

Wanawake wawili toka nchini Marekani wamekamatwa na maofisa wa usalama nchini humo mara baada ya akina mama hao kupekuliwa na kukutwa na madawa ya kulevywa aina ya cocaine yenye thamani ya paundi milioni 2.Wanawake hao wamekamatwa yakiwa yamewekwa kwenye nguo za ndani za akina mama hao wakiwa wamezivalia ila zikiwa ni za bandia.
Pena Prisila na Michelle Blasingale walisimamishwa na maofisa wa Forodha kwenye uwanja wa ndege wa JFK baada ya kutoka Jamuhuri ya Dominika.Maafisa hao baada ya kuwakagua kwenye mizigo yao hawakuweza kuona chochote zaidi walipowakagua kwenye mavazi yao ndipo wakagundua kua walikua wamebeba madawa hayo huku kila mmoja akiwa na madawa zaidi kilo 3.Wanawake hawa wote kutoka Marekani wameweza kufunguliwa mashtaka ila Pena yuko nje kwa dhamana ila mwenzie Michelle yuko rumande.hivi ndivo ilivokua katika picha
nguo za ndani ndivo zilikua kwenye hali hii.




NEEMA WA 20% AWEKEWA MENO YA BANDIA.

Asifa Omary alimaarufu Neema wa 20%,Ni msanii aliye igiza kwenye filamu ambato alijizolea umaarufu kwenye filamu ya ''furaha iko wapi 20%''ambayo aliigiza kama NEEMA.Hivi karibuni amewekewa meno matano ya bandia kutokana na kung'oka kwa meno hayo mara baada zya kuanguka na usafiri maarufu wa mjini ambao uko fasta kama vijana wa mjini wanavosema boda boda.
Alianguka akiwa na kijana mmoja aliejulikana kwa jina la Abdukarim Ally ambae yeye aliweza kuumia juu ya jicho na kupasuka.Wote wamelazwa huku kila mmoja akiwa ameumia na akiwa na maumivu yake.
huyu ndio Neema mwenyewe
akiwa anaugulia maumivu.
Abdukarim Ally.


MWANAMKE MWENYE HIPS KUBWA DUNIANI.

Huyu ndo mwanamama Mikel Ruffineli mkazi wa Los Angels,Marekani.Amedhihirisha kua yeye ndo mwanamke mwenye Hips kubwa Duniani kwa kua ana zaidi ya mzunguko wa futi 8.Mama huyu mwenye watoto wanne hua anapata tabu sana hasa pale anapotakiwa kupita kwenye mlango wa nchi 100 na kama kwenye ndege hukaa nafasi za watu wawili.
Mikel ameendelea kusema kua gari anaendesha kubwa kutoka kwamba magari madogo ya siti au kiti kisicho na uimara ambao hauwezi kumudu uzito wake kwani yeye mwenyewe ana uzito wa kilo 190 na akiwa na umri wa miaka 39.
Mikel Ruffineli akipimwa.
kiti atumiacho akiwa nyumbani.
anasema unene sio sababu ya yeye kuzuiwa kwenda ufukweni kupunga upepo.
Kaongeza kua pamoja na unene huo alionao hakuna mbinu ya zaida ambayo ameifanya ili awe hivyo ila ndo maumbile yake aliyozaliwa nayo kwan tangu alipozaliwa alikua na kilo zipatazo 63 na pia uwezekano wa kufanya upasuaji kwa ajili ya unene huo upo ila sema anajivunia kua mnene na umbo hilo pia kaendelea kusema uzito alionao umeweza kuchangiwa na kua na watoto wanne.





KITALE APATA AVUTA JIKO.

Hapo jana ni siku ya kipekee sana hasa kwa hawa wapendanao ambao wameaamua kufunga pingu za maisha na kuachana na maisha ya ukapela na huyu si mwingine ila ni ndugu Yussuf Mussa Kitale alimaarufu Kitale hapo jana mchana ameweza kufunga pingu hizo na bibie Fatuma Salum Abbas.
Uchumba wa Kitale na bibie huyu ni wa muda mrefu kwani toka shule ya msingi wako pamoja na kufanikiwa kumpata mtoto mmoja waliempa jina la Hemed.
                                                               Picha na Saluti5
katika pozi Kitale na malkia wake.
mwanadada Fatuma akitia saini ya kuthibitisha kua ndoa hio ni halali..
Mungu ailinde ndoa yako ndugu Kitale kwa kumaliza hatua mmoja ya maisha ya binadamu.
baba mzazi wa Kitale.
Bi.Fatuma akiwa na mtoto wao Hemed.




YALIYOJIRI KIGOMA NA MIAKA 36 YA CCM.

Haya ndio yaliyojiri Mkoani Kigoma kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha mapinduzi CCM yaliyoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Ndugu Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.mambo yalianza hivi;
walianza kwa maandamano wote kwa pamoja akiwemo mwenyekiti mwenyewe wa chama na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi.
maandamano yakiendelea yakiongozwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 
Mwenyekiti na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano akiwapungia mkono wananchi wa Kigoma.
viongozi wa juu wa UVICCM taifa 



Mke wa mwenyekiti wa CCM taifa mama Slma Kikwete akiwasalimia wananchi wa mkoa wa Kigoma.