Saturday, February 2, 2013

VALENTINE'S DAY HIIIO UNASEMAJE JUU YA HUU UHUSIANO??

Mahusiano ya Mwanamuziki Naseeb Abdul alimaarufu Diamond na msanii wa filamu nchini Tanzania Wema Isaack Sepetu,unaweza kuyaongeleaje kwa maana kwamba uliyachukuliaje kwa jinsi walivokua wakiishi hapo awali kabla ya kuatengana kutokana na mambo ya hapa na pale hususani katika swala la mapenzi haya mabo hua yapo tu.
Hivo sema chochote kuhusu haya mahusiano ya wema na diamond hasa katika kuelekea siku ya wapendanao duniani ama kwa jina la VALENTINE'S DAY kwa wengi tunavoifahamu.

Diamond & Wema 

KAMA HAUKUONA UANGUKAJI WA STENDI KUU YA MABASI UBUNGO HII HAPA.

Kama haukufanikiwa kuiona kurasa ya juu tukio la stendi ya mabasi ubungo kuangukia magari hii ni fursa yako sasa. kuitizama hapa.

SIRI YA MTUNGI WAENDELEZA HARAKATI ZAO.

Kwa wapenzi na wafuatiliaji wa onesho la Siri ya Mtungi mambo ndo kwanza bado yako motomoto kutokana kwamba vitu vinzidi kunoga siku hadi siku.Kwa wale ambao hawakuweza kuangalia siri ya mtungi sehemu zilizopita mnaweza kutembelea www.siriyamtungi.com na kuweza kuangalia sehemu zote ambazo hukuweza kuziona pia tembelea katika ukurasa wa facebook ambao ni www.facebook.com/siri ya mtungi utaweza kuona yanayojiri siri ya mtungi.




GARI LA MAREHEMU SHARO MILLIONEA LAUZWA.

Mama mzazi wa aliekua msanii wa muziki na filamu hapa nchini marehemu Hussein Ramadhani Mkiety alimaarufu sharo millionea.ameibuka na swala hili mara baada ya arobaini ya marehemu mwanae sharo na kusema kua analiuza gari la mwanae aliloliacha kutokana kwamba hawezi kuliendesha na pia haliwezi kukaa tu bila kufanya kitu hivo basi ameongeza kua hamtambui mwanadada aliejulikana kwa jina la Mary Lucas wa sumbawanga kua ana ujauzito wa marehemu sharo kutokana kwamba enzi za uhai wa mwanae sharo hajawahi kutambulishwa kua ana mpenzi au mchumba hivo huyu dada mimi simtambui.Alimaliza kwa kusema ivo.
Imeripotiwa na Gladness Mallya.

WEMA ACHUKUA FORM YA BBA 2013.

Baada ya kuwepo na tetesi nyingi san mtaani juu ya nani anafaa kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano yanayo fanyika kila mwaka ndani ya jumba kubwa la BBA{Big Brother Africa}.Leo limeanza kutimia mara baada ya mwanadada Wema Isaack Sepetu kuweza kuchukua form hio ndani ya ofisi za multi choice jijini kwa ajili ya mchakato wa BBA 2013.